Mfano wa nadhiri iliyotundikwa na isiyotundikwa

Swali: Ni vipi inakuwa nadhiri ambayo haikutundikwa?

Jibu: Ni kusema ”Ni lazima kwangu kwa ajili ya Allaah kutoa 100 SAR”, ”Ni lazima kwangu kufunga kwa ajili ya Allaah jumatatu na alkhamisi kwa ajili ya Allaah”, hii ni aina ya nadhiri ambayo haikutundikwa. Aina ya nadhiri iliyotundikwa ni kama kusema ”Ni lazima kwangu kwa ajili ya Allaah kufunga mwezi mzima Allaah akimponya mtoto wangu”, ”Ni lazima kwangu kwa ajili ya Allaah kutoa swadaqah kiwango kadhaa Allaah akimrudisha mwanangu kutoka safarini mwake” na ”Ni lazima kwangu kwa ajili ya Allaah mtoto wangu akipasi chuo kikuu”. Hii ni aina ya nadhiri zilizotundikwa.

Swali: Vipi asipopasi chuo kikuu?

Jibu: Hakuna chochote kitachomlazimu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24397/ما-صفة-النذر-المعلق-والنذر-المطلق
  • Imechapishwa: 05/10/2024