Wale ambao yamekamilika matendo na vitendo vyao

Swali: Kunasemwa juu ya wakweli kwamba ni wanazuoni na wenye matendo ilihali Allaah amesema:

وَالَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ أُولَـٰئِكَ هُمُ الصِّدِّيقُونَ

”Na wale waliomuamini Allaah na Mtume Wake, hao ndio wakweli.”[1]

Jibu: Ni wenye imani iliokamilika zaidi kutokana na ukamilifu wa ukweli, maneno na vitendo vyao vinavyoonekana na visivyoonekana. Wakweli ni wale ambao yamekamilika maneno na vitendo vyao katika dini ya Allaah. Wamekuwa katika ngazi ya juu zaidi baada ya Mitume.

[1] 57:19

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah (01)
  • Imechapishwa: 13/05/2024