Swali: Siku zote huenda kuswali Fajr na nakuta swali imekwishaanzwa na mimi nakuwa bado sijaswali Rak´ah mbili za Fajr. Je, inafaa kwangu kuiswali baada ya imamu kutoa Tasliym? Je, kuna chochote katika ujira kinapungua endapo nitasubiri mpaka kuchomoze jua kwa vile Rak´ah mbili za Fajr ni bora kuliko ulimwengu mzima na vilivyomo ndani yake kama ilivyokelewa katika Hadiyth?

Jibu: Kama haikuwa wepesi kwa muislamu kuswali Sunnah ya Fajr kabla ya swalah, basi amepewa khiyari ya kuiswali baada ya swalah au kuichelewesha mpaka baada ya kuchomoza kwa jua. Kwa sababu Sunnah imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa mambo yote mawili. Lakini kuichelewesha ndio bora mpaka baada ya kuchomoza kwa jua. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliamrisha kufanya hivo. Kuhusu kuitekeleza baada ya swalah ni jambo limethibiti kutoka katika kukubali kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kitu kinachofahamisha jambo hilo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/373)
  • Imechapishwa: 08/11/2021