Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Upepo ni katika rehema ya Allaah. Unakuja kwa rehema na unakuja kwa adhabu. Mnapouona msiutukane. Muombeni Allaah kheri yake na muombeni kinga kutokana na shari yake.”[1]

Ameipokea Abu Daawuud.

´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Alikuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) unapokuwa upepo mkali husema:

اللّهُـمَّ إِنَّـي أَسْـأَلُـكَ خَيْـرَها، وَخَيْـرَ ما فيهـا، وَخَيْـرَ ما اُرْسِلَـتْ بِه، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْ شَـرِّها، وَشَـرِّ ما فيهـا، وَشَـرِّ ما اُرْسِلَـتْ بِه

”Ee Allaah! Nakuomba kheri yake, kheri ya kilichomo ndani yake na kheri ya iliyotumwa ndani yake. Na najilinda Kwako kutokamana na shari yake, shari ya kilichomo ndani yake na shari iliyotumwa nao.”[2]

Ameipokea Muslim.

´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

”Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa anaona kutawanyika kwa mawingu katika upeo wa macho anaacha anachokifanya, hata kama ni du´aa, na kusema:

اللهُمَّ إِنِي أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّهَا

“Ee Allaah! Ninakuomba kinga dhidi ya shari yake.”

Kunapoanza kunyesha anasema:

اللَّهُمَّ صيِّباً هَنيئاً

“Ee Allaah! [Ijaalie iwe ni] yenye kumiminika yenye kunufaisha!”[3]

Ameipokea Abu Daawuud.

[1] Abu Daawuud (5097), Ibn Maajah (3727), Ahmad (3/65) na an-Nasaa’iy katika “´Amal-ul-Yawm wal-Laylah” (931-932). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib” (126).

[2] Muslim (899).

[3] Abu Daawuud (5099), Ibn Maajah (3889), Ahmad (8/364) na an-Nasaa’iy katika “´Amal-ul-Yawm wal-Laylah” (914-915). Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh kwa sharti za Muslim kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib” (128).

  • Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 317
  • Imechapishwa: 09/09/2025