Wakati wa Adhaana ya kwanza ya Fajr

Swali: Baadhi wanaadhini adhaana ya Fajr saa moja kabla, wengine masaa mawili na wengine nusu saa. Je, ina wakati maalum?

Jibu: Sunnah ni kwamba ya kwanza iwe muda mfupi kabla ya alfajiri, isiwe kwa muda mrefu sana. Hivo ndivo alivokuwa akifanya Bilaal na Ibn Umm Maktuum, ambapo Bilaal alikuwa akitoa adhaana wakati wa karibu na Fajr. Bora iwe nusu saa, theluthi ya saa au robo saa kabla ya alfajiri. Lengo ni kuwatahadharisha watu kuwa wakati wa Fajr umekaribia. Baadhi ya watu wamejuzisha kuitoa adhaana kutoka katikati ya usiku, lakini hakuna dalili inayothibitisha hilo. Lililo bora zaidi ni kuwa adhaana iwe karibu na alfajiri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24778/متى-وقت-الاذان-الاول-لصلاة-الفجر
  • Imechapishwa: 17/12/2024