Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Anayesema wakati anapotoka nyumbani:

بِسْمِ اللهِ تَوَكَّلْتُ عَلى اللهِ وَلاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ باللهِ تَعَالى

“Kwa jina la Allaah. Ninamtegemea Allaah. Hapana mabadiliko wala uwezo isipokuwa kwa msaada wa Allaah (Ta´ala).”

huambiwa: “Umekingwa, umelindwa na kuongozwa.” Ataokolewa na Shaytwaan na kumwambia Shaytwaan mwengine: “Utamfanya nini mtu ambaye ameongozwa, amekingwa na amelindwa?”[1]

Imekuja kwa Ahmad:

بسم الله آمنت بالله، اعتصمت بالله، توكلت على الله، ولا حول ولا قوة إلا بالله

“Kwa jina la Allaah. Ninamtegemea Allaah. Nimeshikamana na Allaah. Nimemtegemea Allaah. Hapana mabadiliko wala uwezo isipokuwa kwa msaada wa Allaah.”

Hadiyth ni nzuri.

Wale wanne wamepokea ya kwamba Umm Salamah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hajawahi kutoka nyumbani isipokuwa alikuwa anaangalia juu mbinguni na kusema:

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ أَنْ أَضِلَّ أَوْ أُضَلَّ أَو أَزِلَّ أَوْ أُزَلَّ أَوْ أَظْلِمَ أَو أُظْلَمَ أَوْ أَجْهَلَ أَوْ يُجْهَلَ عَليَّ

“Ee Allaah! Najikinga Kwako kutokana na kupotea au kupoteza, kuteleza au kumtelezesha mtu, kudhulumu au kudhulumiwa, kuwa mjinga au kufanywa mjinga.”[2]

at-Tirmidhiy amesema:

”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”[3]

[1] Abu Daawuud (5095), an-Nasaa’iy katika “´Amal-ul-Yawm wal-Laylah” (89) na at-Tirmidhiy (3426), ambaye amesema:

“Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”

[2] Abu Daawuud (3427), at-Tirmidhiy (5094), an-Nasaa’iy (5501), Ibn Maajah (3884) na Ahmad (8/616).

[3] al-Albaaniy sade:

“Mambo ni kama alivosema. Hata hivyo jumla inayosema kuangalia juu mbinguni ni yenye kupingana na zilizo Swahiyh (شاذ). Tazama “as-Swahiyhah” (3193).” (Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib (45)

  • Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 260-161
  • Imechapishwa: 17/09/2025