Zayd bin Khaalid al-Juhaniy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alituswalisha Swalah ya Subh Hudaybiyah baada ya usiku ulionyesha. Wakati alipomaliza aliwageukia watu na kusema: ”Mnajua nini amesema Mola Wenu?” Wakasema: ”Allaah na Mtume Wake ndiyo wenye kujua zaidi.” Akasema: ”Baadhi ya waja wangu wameamka hali ya kuwa ni waumini na wengine makafiri. Waliosema: ”Tumenyeshelezewa kwa sababu ya fadhila na Rahmah za Allaah” wananiamini Mimi na wanakanusha nyota. Ama wale waliosema: ”Tumenyeshelezewa kwa sababu ya nyota kadhaa na kadhaa” anaamini nyota na amenikanusha Mimi.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Imesemekana kwamba kuomba du´aa wakati wa kunyesha mvua ni jambo lililopendekezwa.

´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

”Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa anaona mvua, husema:

اللّهُمَّ صَيِّـباً نافِـعاً

“Ee Allaah! Iteremshe kwa wingi na iwe yenye manufaa!”[2]

Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mvua ilinyesha nasi tukiwa pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akakunja nguo yake ili mvua impate. Tukasema: ”Ee Mtume wa Allaah, kwa nini umefanya hivo?” Akasema: ”Kwa sababu ndio punde imetoka kwa Mola wake.” [3]

Ameipokea Muslim.

[1] al-Bukhaariy (846, 1037 na 4147) na Muslim (71).

[2] al-Bukhaariy (1032).

[3] Muslim (898).

  • Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 320
  • Imechapishwa: 09/09/2025