Swali: Nini maana ya kwamba tawbah inakubaliwa muda wa kuwa mtu hajasagasaga miguu?

Jibu: Maana yake ni kwamba muda wa kuwa haujafika muda wa kukata roho baada ya kumuona Malaika wa kifo.

Swali: Vipi kuhusu maneno yake Fir´awn:

حَتَّىٰ إِذَا أَدْرَكَهُ الْغَرَقُ قَالَ آمَنتُ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا الَّذِي آمَنَتْ بِهِ بَنُو إِسْرَائِيلَ وَأَنَا مِنَ الْمُسْلِمِينَ

”… mpaka ilipomfikia kuzama akasema: ”Nimeamini kwamba hapana mungu wa haki, isipokuwa Yule waliyemwamini wana wa israaiyl, na mimi ni miongoni mwa waislamu.”[1]?

Jibu: Imani yake hii haikumfaa kitu kwa sababu adhabu imeshashuka. Amesema (Ta´ala):

فَلَمَّا رَأَوْا بَأْسَنَا قَالُوا آمَنَّا بِاللَّـهِ وَحْدَهُ وَكَفَرْنَا بِمَا كُنَّا بِهِ مُشْرِكِينَ فَلَمْ يَكُ يَنفَعُهُمْ إِيمَانُهُمْ لَمَّا رَأَوْا بَأْسَنَا

”Walipoiona adhabu Yetu walisema: ”Tumemuamini Allaah pekee na tunayakanusha vile ambavyo tulikuwa tunamshirikisha Naye. Haikuwa imani yao ni yenye kuwafaa pale walipoona adhabu Yetu.”[2]

Adhabu inaposhuka tawbah hainufaishi. Wakati kina Thaamuud na kina ´Aad walipoteremkiwa na adhabu tawbah haikuwanufaisha kitu. Tawbah inakubaliwa kabla ya hapo.

[1] 10:90

[2] 40:84-85

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24572/معنى-تقبل-التوبة-ما-لم-يغرغر
  • Imechapishwa: 04/11/2024