Wakati ambao mume unatakiwa na wakati hutakiwi kumpa ruhusa mke ya kutoka

Swali: Vipi ikiwa atatoka bila idhini yake?

Jibu: Anapaswa kumwongoza na kumfundisha. Ikiwa kutoka kwake kunatokana na manufaa, kama vile kumtembelea mgonjwa au familia yake, basi asitilie mkazo katika jambo hilo. Na ikiwa anatilia mashaka juu ya kutoka kwake, basi amkatalie. Hata hivyo ikiwa kutoka kwake kunakubalika katika Shari´ah na kuna mtazamo wa kukubaliwa, basi hatakiwi mwanaume asitilie mkazo. Baadhi ya watu daima wanakuwa na ususuwavu na dhana mbaya. Ikiwa kutoka kwake mwanamke ni mwema basi haitakiwi kumdhania vibaya. Hapana vibaya ikiwa kutoka kwake kunakubalika katika Shari´ah kwa ajili ya kuwatembelea jamaa zake ndani ya wakati wa sawa au kwenda kwa majirani zake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/29320/ما-المشروع-لمن-خرجت-زوجته-بغير-اذنه
  • Imechapishwa: 02/06/2025