Swali: Je, mtu aache kutendea kazi Sunnah kwa sababu tu watu hawazitambui?

Jibu: Hapana, haitakiwi kufanya hivo. Hata hivyo wanaweza kuwa wenye kupewa udhuru. Ni dhuluma kuwepo kwa wajinga kuwaongoza wanazuoni na kuwaambia wanayotakiwa kufanya na wasiyotakiwa kufanya. Baadhi yao hawawezi hata kusoma Suurah “al-Faatihah” na “al-Falaq” kisahihi. Halafu baada ya hapo wanataka kuwaongoza wanafunzi ambao magoti yao yamekomaa kwa ajili ya kukaa katika vikao vya wanazuoni. Baya zaidi kuliko hilo ni wawaduhumu wa mikahawa wasiokutaka uitendee kazi Sunnah na wanasema:

“Nyinyi Wahhaabiyyah mmetuharibia dini yetu!”

Na ni dini gani ulionayo, ee masikini? Unywaji pombe? Rushwa? Utapeli?

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 399-400
  • Imechapishwa: 25/06/2025