Swali: Baadhi ya watu wa kawaida wanapokutana wanafanyiana laana?

Jibu: Hili ni kutokana na ujinga wao na upumbavu wao. Wanapaswa kupewa nasaha na kuelekezwa katika kheri.

Swali: Vilevile baadhi ya wanawake wanawalaani baba wa watoto wao?

Shaykh: Wote hawa wanafaa kufahamishwa na kubainishiwa kuwa hili ni jambo la maovu. Allaah (‘Azza wa Jall) amesema:

وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَى

“Shirikianeni katika wema na uchaji Allaah.”[1]

وَتَوَاصَوْا بِالْحَقِّ وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ

“… na wakatenda mema na wakausiana kwa haki na wakausiana subira.”[2]

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yeyote katika nyinyi atakayeona maovu miongoni mwenu, basi ayaondoe kwa mkono wake…”

Ni lazima.

[1] 05:02

[2] 103:3

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/27634/ما-حكم-ما-يقع-من-تلاعن-العوام-والازواج
  • Imechapishwa: 06/04/2025