Swali: Ni ipi hukumu ya kuwazika zaidi ya maiti mmoja katika kaburi moja kulifunua kukifungua kaburi pale anapopatikana maiti mwingine wa familia hiyo, kama inavyofanyika katika baadhi ya maeneo?

Jibu: Sunnah ni kwamba kila mtu azikwe katika kaburi lake peke yake. Hivi ndivyo Sunnah na ndivyo ilivyokuwa katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kule al-Baqiy´. Kila mmoja alizikwa kaburi lake pekee, hawakuwekwa wawili au watatu pamoja. Lakini kama kutatokea haja, kwa mfano wakafa watu wengi kwa sababu ya janga, ugonjwa wa kuambukiza au vita vikubwa vikapelekea vifo vingi, basi hakuna ubaya kuwazika wawili au watatu katika kaburi moja. Hivi ndivyo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alivyofanya katika vita vya Uhud, ambapo waliweka wawili au watatu katika kaburi moja. Kwa hivyo kama kutatokea maafa yanayoleta vifo vingi kwa wakati mmoja, hakuna tatizo kuweka maiti zaidi ya mmoja katika kaburi moja.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1167/ما-حكم-وضع-اكثر-من-ميت-في-القبر
  • Imechapishwa: 06/02/2026