Wachumba kuandikiana kabla ya ndoa

Swali: Je, inajuzu mchumba kumwandikia mchumba wake kabla ya kufunga ndoa? Je, uchumba ni jambo linakubalika katika Shari´ah?

Jibu: Hakuna ubaya kumwandikia kwa jambo linalomnufaisha, kama kumpa zawadi au mengineyo. Hapana neno ikiwa uchumba tayari umeshafanyika kati yao au ikiwa anataka kuwahamasisha hilo, basi anaweza kutuma kwa watu wa familia yake au kwake mwenyewe zawadi ili awaombe wakubali ndoa, hakuna ubaya katika hilo. Muhimu ni kwamba hilo lifanyike kwa njia inayokubalika katika Shari´ah, si kwa njia ya faragha wala kwa njia ya kukutana kwa njia mbaya. Bali kwa njia ya kujipendekeza kwa watu wa kwao na kwake yeye kwa zawadi mpaka wakubali ombi lake, hakuna ubaya katika hilo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2268/حكم-مراسلة-الخاطب-لخطيبته-قبل-العقد
  • Imechapishwa: 09/01/2026