Viungo vyote ni lazima vilowe

Swali: Nimesikia kuwa ni lazima maji yachururike juu ya kiungo wakati wa kutawadha, jambo ambalo limenisababishia uzito na kufanya israfu na khaswa wakati wa kuoga. Ni ipi hukumu ya hilo? 

Jibu: Ndio, ni lazima maji yachururike juu ya kiungo. Ikiwa sehemu ya kiungo haikulowa na kupatwa na maji twahara haisihi. Maji ni lazima yaguse kiungo kizima. Ama kuhusu kusugua, hii ni ziada. Inatosheleza kwa maji kulowa kiungo chote.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (29) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%2025-12-1435.mp3