Watu wanatofautiana inapokuja katika vitabu. Mtu wa kawaida anatakiwa kusoma vitabu kama:

1 – Riyaadh-us-Swaalihiyn

2 –”Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym” ya Ibn Kathiyr.

3 – Buluugh-ul-Maraam

4 – Fath-ul-Majiyd Sharh Kitaab-it-Tawhiyd

5 –”ad-Durr an-Nadhwiyd” ya ash-Shawkaaniy.

6 – ”Tatwhiyr-ul-I´tiqaad” ya as-Swan´aaniy.

7 – al-Lu’lu’ wal-Marjaan.

Vitabu hivi mtu wa kawaida anatakiwa kuwa navyo.

Kuhusu ambaye yuko na ngazi ya juu kidogo kuliko mtu wa kawaida anatakiwa kusoma “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy na ya Muslim. Aidha akiweza kupata vile vitabu vya “as-Sunan” ya Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaa´iy na Ibn Maajah, ni jambo zuri. Vitabu hivi vinamsahilishia mtu ambaye anasoma na kuandika na anaipenda elimu.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 494-495
  • Imechapishwa: 10/05/2025