Namshauri aipe umuhimu Qur-aan. Kitabu cha Allaah ndicho kitu muhimu zaidi. Qur-aan Tukufu ndiyo muhimu kuliko yote. Ajishughulishe nacho kwa kuhifadhi na azidishe kukisoma na kutafakari maana yake. Ikiwa hataweza kukihifadhi, basi azidishe kukisoma, kwani kusoma mara nyingi humfanya mtu akikumbuke na awe karibu na wahifadhi. Kwa hiyo ninashauri azidishe sana kusoma Kitabu cha Allaah kwa kutafakari na kukielewa katika nyakati zinazofaa kama mwanzo wa mchana, usiku au mwisho wa usiku. Hivyo atafaulu kuhifadhi Qur-aan au sehemu zake, pamoja na kujali maana na kusoma vitabu vya tafsiri ya Qur-aan, kama “Tafsiyr Ibn Kathiyr”, “Tafsiyr-ul-Baghawiy” na vyenginevyo, ili maarifa yake yawe yenye nguvu na awe juu ya bayana ya Kitabu cha Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).
Kisha Sunnah zake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Nammashauri ahifadhi kile kitakachowezekana, kama “Buluugh-ul-Maraam” ambacho ni kitabu kizuri, kilichohakikishwa na chenye faida. Pia “´Umdah-ul-Ahkaam” cha Shaykh ´Abdul-Ghaniy al-Maqdisiy ambacho asili yake ni kutoka kwa ”as-Swahiyh” ya al-Bukhariy na ya Muslim. Nacho ni kitabu kizuri. Aidha “al-Arba´iyn an-Nawawiyyah”, na “ar-Rahabiyyah”. Akivihifadhi na kuvizingatia itakuwa ni kheri.
Ikiwezekana kupata elimu zaidi na hima yake ikapanda na maarifa yake yakaongezeka, basi ajishughulishe na “Swahiyh-ul-Bukhariy”, “Swahiyh Muslim”, vitabu vya Sunan vinne pamoja na “al-Muwattwa’” cha Imaam Maalik na “al-Musnad” ya Ahmad. Haya yote ni kheri juu ya kheri akishamaliza masomo yake ya msingi na maarifa yake yamesimama vizuri. Ndani yake kuna hazina kubwa mno, humo mna tafsiri ya Kitabu cha Allaah na msaada mkubwa wa kuelewa maneno ya Allaah na maneno ya Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Kisha atilie umuhimu vitabu vya lugha kwa ajili ya kusaidia uelewa wake wa vitabu vya tafsiri na vitabu vya Hadiyth ili vimsaidie katika kufahamu Qur-aan na Sunnah, kutoa msimamo sahihi na kubatilisha yaliyobatilika.
Miongoni mwa vitabu vyenye manufaa makubwa ni “Muntqaa´ al-Akhbaar” cha Ibn Taymiyyah, nacho ni kitabu kikubwa chenye mkusanyiko mzuri wa elimu nyingi, pia “Jaamiy´-ul-Usuwl” cha Ibn-ul-Athiyr, “Zaad-ul-Ma´aad” cha Ibn-ul-Qayyim ambacho ni kitabu bora mno kinachoelezea mwongozo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), “I´laam-ul-Muwaqqi´iyn” cha Ibn al-Qayyim na “Ighaathat-ul-Lahfaan” cha Ibn Al-Qayyim. Vitabu hivi ninavishauri sana kusomwa kwa makini kwa sababu vina manufaa makubwa mno.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1125/نصيحة-للشباب-لتجنب-الافراط-والتفريط
- Imechapishwa: 09/06/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1125/نصيحة-للشباب-لتجنب-الافراط-والتفريط
Imechapishwa: 09/06/2026
https://firqatunnajia.com/vitabu-ambavyo-ibn-baaz-anapendekeza/