28 – Ahmad bin Mihraan al-Faarisiy ametukhabarisha: ´Ubaydullaah bin Sa´iyd bin ´Ufayr ametuhadithia: Baba yangu ametuhadithia… (ح) Ishaaq bin Ibraahiym bin Haashim al-Adhra´iy ametuzindua: Yahyaa bin Ayyuub al-Miswriy ametuhadithia: Yahyaa bin Bukayr ametuhadithia, kutoka kwa Maalik bin Anas, kutokka kwa Zayd bin Abiy Unaysah, ambaye amesimulia kuwa ´Abdul-Hamiyd bin ´Abdir-Rahmaan bin Zayd bin al-Khattwaab amemukhabarisha kwamba Muslim bin Yasaar amemukhabarisha:
”´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) aliulizwa juu ya Aayah hii:
أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ ۖ قَالُوا بَلَىٰ ۛ شَهِدْنَا
“Je, Mimi siye Mola wenu?” Wakasema: “Ndio bila shaka, tumeshuhudia!”
´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) amesema: ”Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiulizwa juu yake, ambapo akasema: ”Allaah (Jalla wa ´Azz) alimuumba Aadam kisha akampangusa mgongo wake kwa mkono Wake wa kuume, akatoa hapo kizazi chake na kusema: ”Hawa Nimewaumba waingie Peponi na watafanya matendo ya watu wa Peponi.” Kisha akampangusa mgongo wake na kutoa hapo kizazi chake na kusema: ”Hawa Nimewaumba waingie Motoni na watafanya matendo ya watu wa Motoni.” Ndipo bwana mmoja akasema: ”Ee Mtume wa Allaah, kwa nini basi tufanye matendo?” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Allaah (´Azza wa Jall) akimuumba mja kwa ajili ya Peponi, basi anamfanya kutenda matendo ya watu wa Peponi, mpaka anakufa juu ya matendo ya watu wa Peponi na hivyo Anamwingiza Peponi kutokana nayo. Na Akimuumba mja kwa ajili ya Motoni, basi anamfanya kutenda matendo ya watu wa Motoni, mpaka anakufa juu ya matendo ya watu wa Motoni na hivyo Anamwingiza Motoni kutokana nayo.”
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 56-57
- Imechapishwa: 09/06/2026
- Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
28 – Ahmad bin Mihraan al-Faarisiy ametukhabarisha: ´Ubaydullaah bin Sa´iyd bin ´Ufayr ametuhadithia: Baba yangu ametuhadithia… (ح) Ishaaq bin Ibraahiym bin Haashim al-Adhra´iy ametuzindua: Yahyaa bin Ayyuub al-Miswriy ametuhadithia: Yahyaa bin Bukayr ametuhadithia, kutoka kwa Maalik bin Anas, kutokka kwa Zayd bin Abiy Unaysah, ambaye amesimulia kuwa ´Abdul-Hamiyd bin ´Abdir-Rahmaan bin Zayd bin al-Khattwaab amemukhabarisha kwamba Muslim bin Yasaar amemukhabarisha:
”´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) aliulizwa juu ya Aayah hii:
أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ ۖ قَالُوا بَلَىٰ ۛ شَهِدْنَا
“Je, Mimi siye Mola wenu?” Wakasema: “Ndio bila shaka, tumeshuhudia!”
´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) amesema: ”Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiulizwa juu yake, ambapo akasema: ”Allaah (Jalla wa ´Azz) alimuumba Aadam kisha akampangusa mgongo wake kwa mkono Wake wa kuume, akatoa hapo kizazi chake na kusema: ”Hawa Nimewaumba waingie Peponi na watafanya matendo ya watu wa Peponi.” Kisha akampangusa mgongo wake na kutoa hapo kizazi chake na kusema: ”Hawa Nimewaumba waingie Motoni na watafanya matendo ya watu wa Motoni.” Ndipo bwana mmoja akasema: ”Ee Mtume wa Allaah, kwa nini basi tufanye matendo?” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Allaah (´Azza wa Jall) akimuumba mja kwa ajili ya Peponi, basi anamfanya kutenda matendo ya watu wa Peponi, mpaka anakufa juu ya matendo ya watu wa Peponi na hivyo Anamwingiza Peponi kutokana nayo. Na Akimuumba mja kwa ajili ya Motoni, basi anamfanya kutenda matendo ya watu wa Motoni, mpaka anakufa juu ya matendo ya watu wa Motoni na hivyo Anamwingiza Motoni kutokana nayo.”
Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 56-57
Imechapishwa: 09/06/2026
Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
https://firqatunnajia.com/12-tunatakiwa-kufanya-matendo/