Vita ya ´Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq na Ihyaa´ at-Turaath dhidi ya Sudan

Nchi za Kiislamu zimekabiliwa na ´Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq, jumuiya yake Ihyaa´ at-Turaath na ´Abdullaah as-Sabt. Kunatolewa pesa ili waipige vita Da´wah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Waache waende Indonesia, Yemen au Sudan. Mnajua wanaitwa vipi Sudan? Watu wa Sudan wanaimuita Muhammad Haashiym al-Hadiyyah na wafuasi wake ambao wanakimbia nyuma ya baadhi ya maslahi ya kidunia na kumfuata ´Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq kuwa ni “Maslahiyyuun” (Wanamaslahi) kwa kuwa wanacholenga tu ni mafanikio ya dunia yao.

Anaharibu – Allaah asimjaze kheri – Da´wah yenye nguvu Sudan. Walikuwa na Da´wah ambayo sisi pia tunataka kuwa nayo. Walikuwa wanaweka kipaza sauti kwenye masoko na kulingania watu huko. Wakati ´Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq alipowaendea, akaanza kuwashughulisha na upigaji kura na demokrasia na kwa njia hiyo Da´wah ikawa imekufa.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbil.net/sounds.php?sound_id=28
  • Imechapishwa: 14/07/2020