Vita dhidi ya ISIS inatakiwa iwe kwa ajili ya Allaah

Ili kutambua kuwa ISIS wana makosa inatosha kama tulivyosema kujua kuwa hawana wanachuoni. Hili tu linatosheleza. Lau wangelikuwa katika kheri, basi wangelikuwa katika njia ya wanachuoni; wanachuoni wa Sunnah na Tawhiyd. Wasingejitosheleza. Allaah (Jall wa ´Alaa) amewafichua katika majanga haya.

Ninawaambia watu wa Libya ya kwamba ni lazima wapambane na kundi hili la kijambazi kwa aina ya njia zote za nguvu endapo kutakuwepo nguvu na uongozi wenye kutambulika. Tangu muda fulani wa nyuma nimesikia kuwa Libya ina jeshi la serikali. Jiungeni na jeshi hili la serikali na linalotambulika ambalo lina uongozi na serikali na ambalo hivi sasa linaita katika kuwapiga vita watenda dhambi hawa. Jiungeni nao. Msifanye upinzani nao pasi na silaha. Kuweni na mapatano na serikali na jeshi lenu. Fanyeni mazoezi na kuweni na silaha na baada ya hapo jiuengeni na watu hawa. Hata kama wanaua baadhi ya watu Sirte lakini kesho – Allaah akitaka – mtashinda kesho. Kuweni na jeshi hili ambalo hivi sasa linaita kupambana nao na jiungeni nao. Jifunzeni namna ya kutumia silaha na kuweni na nia safi.

Hamasisheni vilevile uongozi wa jeshi kuwa na nia safi kwa ajili ya Allaah (Jalla wa ´Alaa). Nia hii inatakiwa iwe kuunusuru Ummah wa Kiislamu wote kutokamana na Khawaarij wote hawa pasi na kujali sawa ikiwa ni ISIS au wengine wowote ambao wanawaua waislamu. Ni juu yenu kuwakumbusha majenerali kuwa na nia safi kwa ajili ya Allaah. Kuna ujira mkubwa katika kuwapiga vita ISIS na watu mfano wao katika Khawaarij:

“Twuubaa kwa yule mwenye kuwaua au kuuawa na wao.”

“Hakika yule mwenye kuwaua ana ujira mkubwa.”

Msiwe na shaka katika kupambana na Khawaarij chini ya maandalizi ya jeshi na yaliyopangwa. Watu hawa wamefanya mazoezi kweli kweli. Msijisalimishe kwenu. Hivi sasa ni lazima kwenu kufanya mazoezi na kujifunza namna ya kutumia silaha.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://ar.miraath.net/fatwah/12009
  • Imechapishwa: 06/11/2016