Vipi nitatambua kuwa ninachokifanya ni dhambi?

Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

27- an-Nawwaas bin Sam’aan (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“… na dhambi ni ile inayoyumbayumba [ulio na mashaka nayo] katika nafsi yako na hupendelei watu waitambue ijapokuwa watu wamekupa shauri lao la Kishari´ah [kukupendelea nacho].”

Ameifasiri dhambi – nayo ni ile yenye kukabiliana na uadilifu – kwa mambo mawili:

1- Kitu cha wazi.

2- Kitu kilichojificha.

Hii ndio mizani ambayo unaweza kuitumia. Naye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni mpole kwa Ummah huu. Amekwambia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“… na dhambi ni ile inayoyumbayumba [ulio na mashaka nayo] katika nafsi yako… “

Hili ni jambo lililojificha.

“… hupendelei watu waitambue… “

Hili ni jambo lililo wazi.

Ukiliendea jambo ambalo linakutatiza na ukapatwa na shaka kama ni jambo la dhambi au la uadilifu na ukayumbayumba nalo na usijue kuwa ni katika dhambi au uadilifu, pamoja na kuongezea juu ya hilo lau utalifanya hutopendelea watu walitambue, basi hii ndio dhambi. Dhambi imekusanyikiwa na mambo mawili:

1- Kitu kilichojificha ambacho kimefungamana na moyo. Nacho ni kwamba unayumbayumba nacho moyoni na moyo una mashaka wa kukifanya.

2- Kitu cha wazi ni kwamba lau atakifanya basi hapendelei watu wakijue. Hii ni sifa kubwa ya (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya uadilifu na dhambi.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 371
  • Imechapishwa: 14/05/2020