Swali: Je, akemewe mwanamke ambaye anafunua uso wake mbele ya wanaume wa kando naye? Wanawake hawa wanachukua baadhi ya maneno ya wanazuoni wanaosema kuwa kuna makinzano kati ya wanazuoni kuhusu mwanamke kufunua uso wake.
Jibu: Kwa njia ya kumnasihi.
Swali: Wanasema kuwa wao wanachukua maoni ya fulani.
Jibu: Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:
وَإِذَا سَأَلْتُمُوهُنَّ مَتَاعًا فَاسْأَلُوهُنَّ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ ۚ ذَٰلِكُمْ أَطْهَرُ لِقُلُوبِكُمْ وَقُلُوبِهِنَّ
“Mnapowauliza basi waulizeni nyuma ya pazia. Hivyo ni utwaharifu zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao.” (33:53)
وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ
“Na wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa kwa waume zao, au baba zao… ” (24:31)
Uso ndio pambo kubwa.
Swali: Je, wakatazwe?
Jibu: Wakatazwe, lakini iwe kwa upole na sio kwa ukali. Wapewe nasaha.
Swali: Kuhusu makinzano kuhusu kufunika uso kwa wanawake, ni maoni yepi yenye nguvu zaidi – kufunika au kufunua?
Jibu: Maoni yenyee nguvu ni kufunika kwa dalili ya Qur-aan.
Swali: Qur-aan imefuta suala la kufunua au kusemwe nini?
Jibu: Qur-aan imebainika kuwa ni wajibu kujisitiri. Mwanzoni wanawake walikuwa wakiruhusiwa kujifunua kisha baadaye Allaah akakataza hilo na kulifuta na kukabaki suala la kujisitiri.
Swali: Kwa hivyo ni lazima kujifunika?
Jibu: Ndio.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24627/كيف-تكون-النصيحة-لمن-تكشف-وجهها
- Imechapishwa: 15/11/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)