Swali: Ni muda kiasi gani ukipita bila kumtembelea ndugu kunazingatiwa ni kukata udugu?
Jibu: Hakuna kikomo maalum. Kuunganisha undugu ni kwa maneno mema, kuwasaidia masikini miongoni mwao, kuwaitikia salamu, kuanza kuwapa salamu na kuwasaidia katika kheri; mambo haya yote ni kuunganisha undugu. Kukata undugu hakuna kikomo maalum. Kuwafanyia ubaridi na ukavu ambao unahesabiwa kuwa kinyume na hali ya kawaida ni aina ya kukata undugu. Kuwafanyia ubaridi na ukavu bila sababu ya Kishari´ah, kuto kutowapa matumizi masikini wao, kutomfanyia wema, kutomsaidia anayedhulumiwa miongoni mwao mpaka apewe haki yake na mfano wa hayo, kunaweza kuhesabiwa kuwa kukata undugu.
Kwa hiyo kukata undugu ni jambo la kidesturi na kimila. Kuunganisha undugu ni jambo la kidesturi na kimila. Yale yanayojulikana kati ya waislamu kuwa ni kuunganisha kizazi, kufanya wema, mawasiliano, salamu na kutenda wema, hayo yanahesabiwa kuwa kuunganisha kizazi. Yale yanayojulikana kati ya waislamu kuwa ni ubaridi na ukavu na kukata kizazi, ndivyo hivyo.
Si muunganisha kizazi yule mwenye kulipiza. Kwa sababu baadhi ya watu wakiona ndugu hawawaungi, basi wao nao hawawaungi na kusema kwamba hawaniungi, hawaji kwangu, basi nami siwaungi. Hili ni kosa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Si muunganisha kizazi yule mwenye kulipiza, bali muunganisha kizazi ni yule ambaye akikatwa undugu naye basi yeye huwaunga.”
Huyo ndiye muunganisha kizazi.
Vilevile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema pale mtu alipomshtakia:
”Ee Mtume wa Allaah! Mimi nina jamaa, nawaunga lakini wao wananikata, nawavumilia lakini wao wananikosea, nawafanyia wema wao wananifanyia ubaya.” Ndipo akasema: ”Ikiwa ni kama ulivyosema ni kama unawalisha majivu ya moto. Utaendelea kuwa pamoja nawe msaada kutoka kwa Allaah juu yao ilimradi uko juu ya hali hiyo njema.”
Basi Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) humsaidia dhidi yao muda wa kuwa anabaki katika hali yake njema. Naye kwa hilo anakuwa ndiye muunganisha kizazi na wao ndio wakatao kizazi. Ama ikiwa wakikuunga nawe unawaunga, na wakikukata nawe unawakata, hapana. Huku si kuunganisha kizazi. Hata mtu asiye ndugu, ikiwa atakuunga na akakufanyia wema, basi inakubidi kumlipiza na kumfanyia wema. Lakini undugu na jamaa wana haki na ziada kuliko hilo. Kwa msemo mwingine unatakiwa kuwaunga hata wakikutaka, unawafanyia wema, unawarudishia salamu, unaanza kuwatolea salamu, unawaalika katika walima na unaitikia mwaliko wao.
Wakikukata kwa sababu ya ugumu wa hali kati yako na wao, chuki au magomvi kwa ajili ya mambo ya dunia, basi unaruhusiwa kuwahama siku tatu tu, si zaidi ya hapo. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hakuna kuhamana zaidi ya siku tatu.”
Kwa hiyo ni lazima kuwa unawaunga baada ya siku tatu, kurejea hali yake ya mwanzo baada ya siku tatu na asiwahame zaidi ya siku tatu. Mbora wao ni yule anayeanza kwa salamu. Mbora wa wawili waliokatana ni yule anayeanza kumtolea mwenzie salamu.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/994/كيف-تكون-صلة-الرحم-وما-هو-حد-القطيعة
- Imechapishwa: 31/12/2025

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/994/كيف-تكون-صلة-الرحم-وما-هو-حد-القطيعة
Imechapishwa: 31/12/2025
https://firqatunnajia.com/vipi-mtu-anaunganisha-undugu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket