Vipi kuoanisha kati ya kuswali Fajr mapema na kuchelewesha?

Swali: Vipi kuoanisha kati ya Hadiyth inayosema:

”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiswali Fajr wakati wa giza la alfajiri.”

na maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yake kupitia yale yaliyopokelewa na watano:

“Chelewesheni Subh mpaka mwone mwangaza, kwani kufanya hivo kuna malipo makubwa.”?

Jibu: Maana yake ni kwamba awe na uhakika. Hivyo asifanye haraka kuswali Subh na asiiweke katika hali ya khatari.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25303/ما-الجمع-بين-حديثي-صلاة-الفجر-بغلس-والاسفار
  • Imechapishwa: 27/02/2025