Swali: Shighaar[1] inajulikana kuwa ni haramu, lakini wapo wawili wameingia humo na sasa wana watoto baada ya miaka tano au saba. Wafanye nini?

Jibu: Wafanye upya ndoa na hakuna kitu juu yao. Wafanye upya ndoa pamoja na kutubia na kuomba msamaha. Ikiwa mke anamkubali mume wake, basi wafanye ndoa upya bila sharti la yule mwanamke mwingine. Afanye mkataba mpya bila sharti la mwanamke mwingine, kila mmoja wao akiwa katika tawbah na msamaha. Yule ambaye hampendi mume wake, basi mume amwache kwa kumpa talaka moja.

Mwanafunzi: Lazima kufanya upya ndoa?

Ibn Baaz: Kila mmoja afanye upya ndoa bila lile sharti ovu, bila sharti la mwanamke wa pili.

[1] Shighaar maana yake ni mwanamume kumuoza ndugu yake wa kike kwa mwanamume mwingine, kwa sharti kwamba mwanamume huyu mwingine naye amuoze ndugu yake wa kike bila mahari yoyote kutoka kwa yeyote kati ya wanawake wawili hao (www.almaany.com)

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/995/كيفية-التخلص-من-زواج-الشغار
  • Imechapishwa: 24/12/2025