Swali: Mtu akisema maneno ya ukafiri na asiyaitakidi. Lakini amseme hivo kwa sababu alikuwa amesahau au amekosea. Ni ipi hukumu yake?

Jibu: Sielewi kusema kwamba amesahau. Ni vipi atasahau? Ama kusema kwamba amekosea, bi maana ni mjinga, ni jambo linawezekana. Inawezekana kweli akawa ni mjinha. Lakini kusema kwamba amesahau… huyu kama alikuwa amelala au ametokwa na akili na akawa amezungumza pasi na kujua, huyu anapewa udhuru. Kwa sababu hana fahamu na katika hali hii ´ibaadah inakuwa si yenye kumuwajibikia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/01.mp3
  • Imechapishwa: 05/08/2018