Swali: Kilichotolewa baharini kinatolewa zakaah?

Jibu: Hakina zakaah kwa mujibu wa maoni sahihi. Lakini kikizungukiwa na mwaka huku mmiliki wake amekiandaa kwa ajili ya biashara, basi kinakuwa ni katika mali za biashara. Ikiwa ni dhahabu au fedha, basi ni lazima kuvitolea zakaah vikizungukiwa na mwaka. Ama ikiwa kilichotolewa baharini si dhahabu wala fedha na mmiliki amekiandaa kwa ajili ya biashara, basi kinakuwa katika mali za biashara.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31325/هل-في-المستخرج-من-البحر-زكاة
  • Imechapishwa: 19/10/2025