Vichinjwa vya mayahudi na manaswara ambavyo mtu hajui hali yake

Swali: Ni ipi hukumu ya kula nyama zinazotoka kwa Ahl-ul-Kitaab ilihali hali zao hazijulikani?

Jibu: Ikiwa wanachinja kwa njia ya Kishari´ah Allaah ametuhalalishia vichinjwa vyao. Na ikiwa hawachinji kwa njia ya Kishari´ah, na wewe ukawa unajua hili, usile. Hata muislamu akichinja kwa njia isiyokuwa ya Kishari´ah sio halali kula kichinjwa chake.

Kuhusiana na kichinjwa usichojua kama kinachinjwa kwa njia ya Kishari´ah au isiyokuwa ya Kishari´ah, bora zaidi jiepushe nacho kwa njia ya kujiepusha na yenye kutia mashaka.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (26) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathul%20%20-%204%20-%201%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 11/02/2017