Swali: Ni ipi hukumu ya kuhudhuria Khutbah ya ijumaa na ni ipi dalili?
Jibu: Inampasa muumini anapomsikia muadhini basi aharakie kujielekeza msikitini ili asikie Khutbah na aswali. Makusudio ya Khutbah ni kuwakumbusha waislamu, kuwasomesha na kuwapa mawaidha. Kwa hivyo ni wajibu aharakie kuhudhuria ili afaidike na mafunzo ya Khatwiyb na pia kuswali kuanzia mwanzo wake bila kupitwa na jambo lolote. Kwa ajili hiyo amesema (Jalla wa ´Alaa):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَاةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ
“Enyi walioamini! Inaponadiwa kwa ajili ya swalah siku ya ijumaa, basi kimbilieni kumtaja Allaah.”[1]
Kwa hiyo ni wajibu kuharakia mara tu baada ya kusikia adhaana. Akiharakisha mapema zaidi ni bora. Kama ilivyothibiti katika Hadiyth Swahiyh ambapo amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kwamba aliyetangulia kwenda ijumaa mapema ni kama aliyechinja ngamia, kisha anayefuata ni kama aliyechinja ng’ombe, kisha anayefuata ni kama aliyechinja kondoo mwenye pembe, kisha anayefuata ni kama aliyechinja kuku na katika saa ya tano ni kama aliyejitolea yai.
[1] 62:9
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30993/ما-حكم-حضور-الخطبة-يوم-الجمعة
- Imechapishwa: 20/09/2025
Swali: Ni ipi hukumu ya kuhudhuria Khutbah ya ijumaa na ni ipi dalili?
Jibu: Inampasa muumini anapomsikia muadhini basi aharakie kujielekeza msikitini ili asikie Khutbah na aswali. Makusudio ya Khutbah ni kuwakumbusha waislamu, kuwasomesha na kuwapa mawaidha. Kwa hivyo ni wajibu aharakie kuhudhuria ili afaidike na mafunzo ya Khatwiyb na pia kuswali kuanzia mwanzo wake bila kupitwa na jambo lolote. Kwa ajili hiyo amesema (Jalla wa ´Alaa):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَاةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ
“Enyi walioamini! Inaponadiwa kwa ajili ya swalah siku ya ijumaa, basi kimbilieni kumtaja Allaah.”[1]
Kwa hiyo ni wajibu kuharakia mara tu baada ya kusikia adhaana. Akiharakisha mapema zaidi ni bora. Kama ilivyothibiti katika Hadiyth Swahiyh ambapo amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kwamba aliyetangulia kwenda ijumaa mapema ni kama aliyechinja ngamia, kisha anayefuata ni kama aliyechinja ng’ombe, kisha anayefuata ni kama aliyechinja kondoo mwenye pembe, kisha anayefuata ni kama aliyechinja kuku na katika saa ya tano ni kama aliyejitolea yai.
[1] 62:9
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30993/ما-حكم-حضور-الخطبة-يوم-الجمعة
Imechapishwa: 20/09/2025
https://firqatunnajia.com/uwajibu-wa-kuharakisha-kwenda-msikitini-mapema-siku-ya-ijumaa/