Swali: Mtu aliweka nadhiri kwa ajili ya Allaah kwamba atachinja kondoo/mbuzi kumi. Baada ya kuchinja alichoweka nadhiri yake, akala katika wawili kati ya hao. Je, kula kwake huku kunajuzu? Ikiwa hakujuzu analazimika kuchinja kondoo wawili wengine badala ya wale alikula?

Jibu: Ikiwa alikusudia tangu mwanzo kwamba atakula katika hao, basi hapana neno juu yake. Lakini kama hakunuia, basi atalipa kiasi cha nyama alichokula. Atanunua sokoni nyama kwa kiwango alichokula na ataitoa kuwapa masikini. Haimlazimu kuchinja kondoo wawili. Bali ni kulipa thamani ya alichokula – kilo, nusu kilo au kiwango anachodhania alikula – anunue kutoka sokoni na atoe swadaqah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30992/هل-يجوز-لصاحب-النذر-الاكل-منه
  • Imechapishwa: 20/09/2025