Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

يَكَادُ الْبَرْقُ يَخْطَفُ أَبْصَارَهُمْ ۖ كُلَّمَا أَضَاءَ لَهُم مَّشَوْا فِيهِ وَإِذَا أَظْلَمَ عَلَيْهِمْ قَامُوا ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَذَهَبَ بِسَمْعِهِمْ وَأَبْصَارِهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

“Unakaribia umeme kunyakua macho yao, kila unapowaangazia basi hutembea humo na unapowafanyia kiza husimama na endapo Allaah angelitaka basi angeliwaondoshea usikivu wao na uoni wao; kwani hakika Allaah juu ya jambo ni muweza.”[1]

Hakika Allaah juu ya kila jambo ni muweza na hashindwi na kitu. Katika uwezo Wake ni kwamba anapotaka kitu basi hukifanya bila kipingamizi wala kikwazo.

Katika Aayah hii na nyenginezo mfano wake kuna Radd kwa Qadariyyah wanaosema kuwa matendo yao si yenye kuingia ndani ya uwezo wa Allaah. Matendo yao yanaingia ndani ya jumla ya maneno Yake:

إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

“Kwani hakika Allaah juu ya jambo ni muweza.”

[1] 02:20

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taysiyr-ul-Kariym, uk. 35
  • Imechapishwa: 08/05/2020