Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Kutabasamu usoni mwa ndugu yako ni swadaqah.”

Je, hii ni dalili ya kwamba mtu asitabasamu usoni mwa mshirikina au kafiri?

Jibu: Mshirikina inatakiwa kumuonyesha ushupavu, chuki na kumdhihirishia kujitenga. Mapenzi, tabasamu na ushirikiano yanakuwa kati ya waislamu. Hayo yanakuwa baina ya waislamu. Lakina kwa makafiri ni chuki, bughudha na uadui; isipokuwa wakati mtu anatarajia manufaa kama vile kuzilainisha nyoyo zao kwa ajili ya kuwalingania kwa Allaah. Katika hali hiyo hapana vibaya.

Swali: Kwa hiyo inafaa kutabasamu usoni mwake kwa ajili ya kumlingania katika dini ya Allaah?

Jibu: Hapana vibaya. Hapana vibaya kwa ajili ya kumlingania kwa Allaah pale atakapoona manufaa ya kufanya hivo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24596/حكم-التبسم-في-وجه-الكافر-للدعوة
  • Imechapishwa: 08/11/2024