Abu Ja´far Muhammad bin al-Hasan bin Haaruun bin Badiynaa amesema:
“Nilisema kumwambia Abu ´Abdillaah Ahmad bin Hanbal (Radhiya Allaahu ´anh): “Nimefika Mosul. Katika mji wetu wengi wao ni Jahmiyyah na ni wachache ambao ni Ahl-us-Sunnah wanaokupenda. Katika mji kumetokea fitina ya al-Karaabiysiy; matamshi yangu ya Qur-aan yameumbwa.” Abu ´Abdillaah akanambia: “Ninakutahadharisha na huyu al-Karaabiysiy, ninakutahadharisha na huyu al-Karaabiysiy. Usizungumze naye na wala usimgumzishe yule mwenye kuzungumza naye.” Alisema hivo mara nne. Nikasema: “Ee Abu ´Abdillaah! Hivi unaonelea kuwa maoni haya yanatokamana na ´Aqiydah ya Jahmiyyah?” Akasema: “Yote haya yanatoka kwa Jahmiyyah.”
- Muhusika: Imaam Abuul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Twabaqaat-ul-Hanaabilah (2/281)
- Imechapishwa: 10/06/2017
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)