Usiweke “Kwanini” au “Vipi” katika makadirio ya Allaah       

Imaam at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Kwa kuwa Allaah (Ta´ala) ameificha elimu ya Qadar kwa viumbe Wake.”

Hakuna yeyote anayejua hilo, si Malaika aliye karibu wala Mtume aliyetumwa. Hawajui hekima ya kuumbwa huyu, kumfanya huyu akawa tajiri na yule akawa fakiri, kumpotosha huyu na kumwongoza huyu, kwa nini huyu anaisha muda mrefu pengine miaka mia moja na ishirini, mwingine anakufa akiwa na miaka arobaini, mwingine chini ya hapo, mwingine anakufa akiwa mtoto na mwingine anakufa akiwa tumboni mwa mama yake. Usipingane nayo na ukasema “Ni kwa nini?” “Vipi iweje?” Hii ni siri ya Allaah ambayo ameificha kwako na ameificha vilevile kwa viumbe na watu. Yeye ni Mwenye hekima kamili (Subhaanah). Anahukumu kwa ayatakayo na kufanya ayatakayo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/370)
  • Imechapishwa: 21/05/2020