Swali: Kuna mtu amewazuia watu njia kwa gari yake, ambapo akaja mtu na kumlaani kutokana na maudhi aliyosababisa, na kwa ajili hiyo anastahiki kulaaniwa. Je, ni sahihi?

Jibu: Ndio. Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

”Bwana mmoja alisema: ”Ee Mtume wa Allaah! Kuna jirani anayeniudhi.” Akasema: ”Nenda utoe samani zako barabarani.” Akaenda na kutoa samani zake njiani. Watu wakamkusanyikia na kusema: ”Una nini wewe?” Akasema: ”Nina jirani anayeniudhi. Nikamweleza hilo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye akasema: ”Nenda utoe samani zako barabarani.” Ndipo wakaanza kusema: ”Ee Allaah, mlaani! Ee Allaah, mfedheheshe!” Alipofikiwa na khabari hiyo, akamwendea na kusema: ”Rejea nyumbani kwako. Naapa kwa Allaah sintokuudhi!”[1]

Yeye mwenyewe ndiye kasababisha. Hiyo ni adhabu yake.

[1] al-Adab al-Mufrad (124). Nzuri na Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (41)
  • Imechapishwa: 28/06/2024