Wanazuoni waliofeli hawawaelekezi watu katika kheri. Wanachojali ni manufaa yao. Wakati tulipokuwa tunasoma katika chuo kikuu cha Kiislamu, kuna mwalimu wetu mmoja alitwambia:
“Enyi wanangu vipenzi! Msiharamishe picha. Mkiharamisha picha basi mtawaweka watu katika uzito.”
Ametakasika Allaah na mapungufu! Masikini! Sisi ndio wenye haki ya kuhalalisha na kuharamisha au ni Allaah (´Azza wa Jall)? Sisi hatuna la kusema. Hatuwezi kusema jambo fulani kuwa ni halali au haramu pasi na dalili kutoka ndani ya Qur-aan na Sunnah. Je, sisi ni wenye huruma zaidi juu ya waja wa Allaah kuliko Allaah ambaye amesema:
وَمَا كَانَ رَبُّكَ نَسِيًّا
“Mola wako si Mwenye kusahau kabisa?”[1]
Si ingeliwezekana kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kusema:
“Allaah amewalaani watengeneza picha – isipokuwa katika zama za mwisho.”
Si angeliweza kusema:
“Malaika hawaingii nyumba ilio na picha – isipokuwa katika zama za mwisho.”
Miongoni mwa ujanja wa wafeliji hawa, ambao daima hujilinda kwa maoni. Sisi tunawaambia:
“Yule anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho basi azungumze kheri au anyamaze.”[2]
Ni lazima kuwatambua Ahl-us-Sunnah na Kundi lililookoka ili uwaulize kuhusu dini hii.
[1] 19:64
[2] al-Bukhaariy na Muslim.
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 313
- Imechapishwa: 19/05/2025
Wanazuoni waliofeli hawawaelekezi watu katika kheri. Wanachojali ni manufaa yao. Wakati tulipokuwa tunasoma katika chuo kikuu cha Kiislamu, kuna mwalimu wetu mmoja alitwambia:
“Enyi wanangu vipenzi! Msiharamishe picha. Mkiharamisha picha basi mtawaweka watu katika uzito.”
Ametakasika Allaah na mapungufu! Masikini! Sisi ndio wenye haki ya kuhalalisha na kuharamisha au ni Allaah (´Azza wa Jall)? Sisi hatuna la kusema. Hatuwezi kusema jambo fulani kuwa ni halali au haramu pasi na dalili kutoka ndani ya Qur-aan na Sunnah. Je, sisi ni wenye huruma zaidi juu ya waja wa Allaah kuliko Allaah ambaye amesema:
وَمَا كَانَ رَبُّكَ نَسِيًّا
“Mola wako si Mwenye kusahau kabisa?”[1]
Si ingeliwezekana kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kusema:
“Allaah amewalaani watengeneza picha – isipokuwa katika zama za mwisho.”
Si angeliweza kusema:
“Malaika hawaingii nyumba ilio na picha – isipokuwa katika zama za mwisho.”
Miongoni mwa ujanja wa wafeliji hawa, ambao daima hujilinda kwa maoni. Sisi tunawaambia:
“Yule anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho basi azungumze kheri au anyamaze.”[2]
Ni lazima kuwatambua Ahl-us-Sunnah na Kundi lililookoka ili uwaulize kuhusu dini hii.
[1] 19:64
[2] al-Bukhaariy na Muslim.
Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 313
Imechapishwa: 19/05/2025
https://firqatunnajia.com/usiwatie-watu-uzito/