Swali: Mwanamke anamtembelea jirani yake mida ya asubuhi bila ruhusa?
Jibu: Asitoke isipokuwa kwa idhini yake. Lakini akimpa ruhusa, mwanaume asitie uzito sana katika suala hilo.
Swali: Vipi ikiwa hakumpa ruhusa?
Jibu: Hatakiwi kutoka nje bila ya ruhusa yake. Hata hivyo kusiwe kuna madhara yoyote. Ikiwa kuna haja basi awatembelee majirani wake wazuri na familia yake. Yeye haichukulii hii kwa uzito sana. Asimtilie uzito sana. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Wabora katika nyinyi ni wale walio bora kwa familia zao na mimi ni mbora wenu kwa familia yangu.”
Imekuja katika Hadiyth nyingine:
“Walio bora zaidi katika nyinyi ni wale ambao ni bora kwa wake zao. Wema ni tabia njema.”
Kukunja uso na kuwa mkali sana si katika maadili mema.
Swali: Hata na dada wa kike?
Jibu: Ndiyo, hapana neno wakiwa ni wema. Hapana vibaya ikiwa nyumba zao ni nzuri. Kuhusu nyumba mbaya asimpe idhini ya kuziingia.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/29319/حكم-من-تزور-جارتها-بدون-اذن-زوجها
- Imechapishwa: 01/06/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket