Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali katika msikiti wa al-Husayn nchini Misri, ilihali inajulikana kuwa al-Husayn bin ´Aliy hakuzikwa nchini humo na kaburi hilo huwa tupu?

Jibu: Maadamu kwao kuna madhihirisho ya al-Husayn, mwito ni kwa jina la al-Husayn au kuna kaburi la al-Husayn, basi haijuzu kwa muislamu kuwaunga mkono katika jambo hilo. Hivyo asiswali humo wala asilihesabu kuwa ni swalah, kwa sababu madhihirisho yako wazi, ni mamoja iwe ni katika kaburi la al-Husayn au kaburi jingine.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/236)
  • Imechapishwa: 01/03/2026