Swali: Wakati mwingine mtu hupita kwenye maovu yanayofanya moyo kuungua, lakini hawezi kuyakemea kwa sababu ya udhaifu wa mwonaji na nguvu ya mfanyaji. Afanye nini katika hali kama hii?
Jibu:
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ
”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yule katika nyinyi atakayeona maovu, basi ayakemee kwa mkono wake. Asipoweza, afanye hivo kwa ulimi wake. Asipoweza, basi afanye hivo kwa moyo wake – na hiyo ni imani dhaifu kabisa.”
Ikiwa mtu yupo katika mazingira ambayo hawezi kuzuia kwa mkono wala kwa ulimi, basi ajiepushe nayo na asihudhurie mahali pa maovu. Bali ajitenge na akemee kwa moyo wake. Lakini akiwa katika mazingira anapoweza kukemea kwa ulimi wake, basi akemee kwa ulimi. Akiwa na uwezo wa kukemea kwa mkono wake, kama vile baba kwa watoto wake, mtawala, kiongozi au mwenye mamlaka, basi akemee kwa mkono wake kulingana na mamlaka aliyo nayo.
[1] 64:16
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30999/ما-حكم-عدم-انكار-المنكر-لقوة-الفاعل
- Imechapishwa: 20/09/2025
Swali: Wakati mwingine mtu hupita kwenye maovu yanayofanya moyo kuungua, lakini hawezi kuyakemea kwa sababu ya udhaifu wa mwonaji na nguvu ya mfanyaji. Afanye nini katika hali kama hii?
Jibu:
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ
”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yule katika nyinyi atakayeona maovu, basi ayakemee kwa mkono wake. Asipoweza, afanye hivo kwa ulimi wake. Asipoweza, basi afanye hivo kwa moyo wake – na hiyo ni imani dhaifu kabisa.”
Ikiwa mtu yupo katika mazingira ambayo hawezi kuzuia kwa mkono wala kwa ulimi, basi ajiepushe nayo na asihudhurie mahali pa maovu. Bali ajitenge na akemee kwa moyo wake. Lakini akiwa katika mazingira anapoweza kukemea kwa ulimi wake, basi akemee kwa ulimi. Akiwa na uwezo wa kukemea kwa mkono wake, kama vile baba kwa watoto wake, mtawala, kiongozi au mwenye mamlaka, basi akemee kwa mkono wake kulingana na mamlaka aliyo nayo.
[1] 64:16
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30999/ما-حكم-عدم-انكار-المنكر-لقوة-الفاعل
Imechapishwa: 20/09/2025
https://firqatunnajia.com/usipoweza-kukemea-maovu-kwa-mkono-wako/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket