Swali: Vijana wengi wamejitoa katika uanachama wa chama cha Iswlaah cha kiyemeni baada ya kutambua haki. Je, una chochote cha kuwaambia?

Jibu: Nawashukuru kwa msimamo huo. Ulaghai umekwisha. al-Ikhwaan al-Muslimuun wanasema katika Khutbah zao:

“Asiyejiunga na chama ni mnafiki.”

Wanasema pia kwamba asiyejiunga na chama ni kama ambaye haswali. Sisi tunashauri kwa kiasi tunachoweza. Mimi nawanasihi kama alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Muumini hadonolewi kwenye shimo moja mara mbili.”[1]

Wasiache chama na kwenda kwenda kujiandikisha katika chama cha ujamaa, jumuiya ya al-Hikmah au kitu kingine. Suburini, enyi wanafunzi! Hakika hamtopata elimu isipokuwa kwa subira. Someni maisha ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtanusuru Uislamu kwa majengo, magari na mambo mengine ya kilimwengu? Au kunusuru Uislamu inakuwa kwa wanaume wa kweli,  wenye kumtakasia nia Allaah na wenye subira? Kwa hiyo nawashauri kusoma maisha yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake. Wamche Allaah katika maisha yao. Umri wako ndio rasilimali yako. Usihatarishe maisha yako.

[1] al-Bukhaariy (6133).

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 354
  • Imechapishwa: 16/06/2025