Usimtii kiumbe yeyote katika kumuasi Muumba

Swali: Ni upi usahihi wa Hadiyth isemayo:

“Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba.”?

Jibu: Zote ni Swahiyh. Hadiyth ni Swahiyh:

“Hakika si vyenginevyo utiifu ni katika yaliyo mema.”

“Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba.”

Kwa hiyo haijuzu kumtii baba, mume, kiongozi au mtawala katika kumuasi Allaah. Ikiwa mtawala, kiongozi, baba au mume akamwambia mtu anywe pombe, basi hatamtii katika hilo.

Swali: Vipi katika kisichokuwa kunywa pombe kama vile akamwambia anyoe ndevu?

Jibu: Au akamwambia anyoe nyoa ndevu zake, mtukane baba yako, mtukane mama yako au usimtii baba yako na wala usiwatii mama yako – mambo haya yote hayapaswi kumtii katika hayo. Au akamwamuru asiswali kwa mkusanyiko.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2600/الحكم-على-حديث-لا-طاعة-لمخلوق-في-معصية-الخالق
  • Imechapishwa: 28/03/2026