Swali: Amesema (Ta´ala):
وَأَمَّا السَّائِلَ فَلَا تَنْهَرْ
“Na mwombaji usimkemee.”[1]
Je, ni maalum kwa anayeomba pesa au ni yenye kuenea?
Jibu: Udhahiri wa Aayah ni yenye kuenea. Karibu zaidi ni kuhusu pesa. Lakini inajumuisha kwa kuenea kwake anayeuliza kuhusu elimu. Waombaji wanatafautiana. Akitambua kuwa mwombaji si muhitaji basi amkemee. Asipojua hali basi asimkemee. Kwa sababu pengine ni mwenye kuhitaji. Muulizaji kuhusu elimu ikiwa malengo yake ni kufaidika basi asimkemee. Na ikiwa malengo yake ni kuchupa mpaka, basi hili n jambo lingine.
[1] 93:10
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (22)
- Imechapishwa: 27/10/2021
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)