Maimamu wanapata uzito na “as-Sajdah” na “al-Insaan” katika Fajr

SwaliBaadhi ya maamuma wanachoshwa kusoma Suurah “as-Sajdah”  na Suurah “ad-Dahr” katika Fajr ya siku ya ijumaa kutokana na urefu wazo. Imamu achukue msimamo gani kwa sababu baadhi wanataka hivo na wengine hawataki?

Jibu: Hii ni Sunnah iliyothibiti kutoka kwa Mutme (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Imewekwa katika Shari´ah kwa imamu kusoma Suurah mbili hizi katika Fajr ya ijumaa ijapo watachukia baadhi ya watu kutokana na uvivu wao. Sunnah ni yenye kutangulizwa mbele ya wote. Kilichosuniwa kwa maimamu katika swalah zote wachunge kutendea kazi Sunnah na kuihifadhi. Amesema (´Azza wa Jall):

لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ

“Hakika mna kigezo chema kwa Mtume wa Allaah.” (33:21)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atakayezipa mgongo Sunnah zangu, basi huyo si katika sisi.”[1]

[1] al-Bukhaariy (5063) na Muslim (1401).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/393-394)
  • Imechapishwa: 27/10/2021