Usikunje mikono ya nguo wakati wa kuswali

Swali: Je, ni sahihi kukunja mikono ya nguo kabla ya kuanza kuswali?

Jibu: Hapana, mtu anatakiwa kuiacha mikono ya nguo yake wazi wakati wa kuingia ndani ya swalah. Haitakiwi kuikunja ili iweze kusujudu pamoja naye.

Swali: Vipi kuhusu kufunga Ghutrah?

Jibu: Vivyo hivyo Ghutra inapaswa kuachwa kama ilivyo.

Swali: Vipi ikiwa mtu atafanya hivyo?

Jibu: Haitakikani kufanya hivyo. Dogo kabisa liwezalo kusemwa ni kwamba jambo hilo linachukiza.

Swali: Vipi ikiwa sehemu ya katikati ya nguo au bisi inasambaa na kuwagusa watu walio karibu wakati wa kusujudu?

Jibu: Hapana, aikusanye karibu naye ili asiwaudhi wengine. Hii ni muhimu, kama ilivyopokewa katika Hadiyth ya Waaa-il bin Hujr, ambapo alipoenda katika Rukuu´ alitoa mikono yake kutoka chini ya vazi lake, akainua mikono yake, na kisha akaiingiza tena baada ya kuinuka, khaswa wakati wa baridi au hali kama hiyo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24850/حكم-كف-الثياب-في-الصلاة-وقبلها
  • Imechapishwa: 01/01/2025