Swali: Ibn Mas’uud (Radhiya Allaahu ´anh) aliposema:

”Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa hai tulikuwa tukisema:

السلام عليك أيها النبي و رحمة الله و بركاته

“Amani, rehema na baraka za Allaah ziwe juu yako, ee Mtume!”

Lakini baada ya yeye kufariki tukawa tunasema:

السلام على النبي

“Amani iwe juu ya Mtume.”

Jibu: Hapana, hiyo ni katika Ijtihaad ya Ibn Mas´uud. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwafundisha na hakuwambia hivo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwafunza waseme:

السلام عليك أيها النبي و رحمة الله و بركاته

“Amani, rehema na baraka za Allaah ziwe juu yako, ee Mtume!”

Licha ya kwamba alijua kuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) atakufa. Isitoshe wakati mwingine wanasema hivo wakiwa mbali na yeye; walioko ´Iraaq, Shaam, Yemen na Makkah wanasema hivo ilihali wako mbali naye. Kwa hivyo ni bora mtu aendelee kusema kama alivyoelekezwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

السلام عليك أيها النبي و رحمة الله و بركاته

“Amani, rehema na baraka za Allaah ziwe juu yako, ee Mtume!”

Hata hivyo, ikiwa mtu atasema:

السلام على النبي

“Amani iwe juu ya Mtume.”

kama alivyosema Ibn Mas’uud,  hapana vibaya. Lakini Sunnah ni kufuata matamshi ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwafunza Maswahabah zake. Kufanya hivo ni bora zaidi kuliko Ijtihaad ya Ibn Mas´uud.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24855/حكم-السلام-عليك-ايها-النبي-بعد-موتهﷺ
  • Imechapishwa: 01/01/2025