Nawanasihi waislamu wote kwa jumla na khaswa Salafiyyuun walioko Senegal juu ya kumcha Allaah (´Azza wa Jall) na kumtakasia nia Allaah katika mambo na hali zao zote. Msimamo wao wakati wa fitina unatakiwa kuwa msimamo wa Salafiyyuun na maimamu wa Uislamu uliojengeka juu ya Qur-aan na Sunnah. Katika msimamo huo inahusiana vilevile na kuthibitisha kwanza inapokuja katika matusi kwa Salafiyyuun na watu wengineo. Ni lazima kwa mtu kuthibitisha kwanza na kuomba dalili.

Matusi yao leo yaliyowafarikisha Salafiyyuun na kuwatawanyisha kutoka kwa baadhi ya watu ni batili, hayakusimama katika chochote katika dalili na ni yenye kwenda kinyume na mfumo wa Salaf. Bali huenda hata wale wengine wakaona haya kutokamana na usulubu kama huu.

Kwa ajili hiyo nawausia Salafiyyuun Senegal wajenge udugu kati yao na wasikubali maneno ya yeyote yule ambaye anawaponda wengine isipokuwa awe na dalili za wazi na bainifu. Ama kuponda tu pasi na dalili ni dhuluma na ni sababu hata ya watu wa Bid´ah kutokukubali. Mcheni Allaah na piteni juu ya mfumo wa Salaf kwa njia ya kwamba msikubali matusi kutoka kwa yeyote juu ya mtu au makundi isipokuwa kwa dalili na hoja. Uhakika wa mambo ni kwamba mnatakiwa kumrudishia batili zake.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=Qzi18ds3xLk&feature=youtu.be
  • Imechapishwa: 15/02/2019