Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

سَلَامٌ هِيَ حَتَّىٰ مَطْلَعِ الْفَجْرِ

”Ni amani mpaka kuchomoza alfajiri!”[1]

Usiku huu ni wenye amani. Allaah (Ta´ala) ameusifu hivo kutokana na wingi wa wale wanaosalimishwa kutokamana na madhambi na kuadhibiwa katika usiku huo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule atakayesimama kuswali usiku wa Qadr kwa imani na kwa matarajio, basi atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia.”[2]

Hapana shaka kwamba kusamehewa kwa madhambi ni salama kutokamana na adhabu zake.

حَتَّىٰ مَطْلَعِ الْفَجْرِ

“… mpaka kuchomoza alfajiri!”

Katika usiku huo Malaika hushuka mpaka kupambazuke alfajiri. Kunapochomoza alfajiri basi usiku wa Qadr unakwisha.

[1] 97:5

[2] al-Bukhaariy (2014) na Muslim (760).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tafsiyr al-Qur-aan al-Kariym, Juz’ ´Amma, uk. 276
  • Imechapishwa: 14/05/2020