Swali: Kuna bwana mmoja Kuwait kwa jina Muhammad al-Hamuud an-Najdiy anasema kuwa haitakiwi kwa mwanafunzi kukosa katika kabati ya vitabu vyake kitabu “Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan” cha Sayyid Qutwub. Je, tuwaache vijana waende katika darsa zake?

Jibu: Naomba kinga kwa Allaah kutokamana na upofu! Namuomba Allaah msamaha na usalama! Vipi mwanafunzi asikose “Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan” iliyoandikwa na mtu ambaye anawakufurisha waislamu na kusema kuwa wameritadi? Namuomba Allaah ulinzi kutokamana na upotevu huu. Huyu ni mpofu. Mwanafunzi hatakiwi kwenda katika darsa kama hizi.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fath-ur-Rahiym al-Waduud, uk. 274
  • Imechapishwa: 19/06/2020