Usiache matendo kwa ajili ya kuogopa watu

Swali: Ni ipi hukumu ya kufanya matendo kwa ajili ya watu?

Ibn Baaz: Kufanya matendo kwa ajili ya watu au kuacha kufanya ´ibaadah?

Muulizaji: Kuacha kufanya ´ibaadah?

Jibu: Hapana. Mtu anatakiwa kufanya matendo na wala asimjali mtu yeyote. Apambane na nafsi yake kumtakasia nia Allaah. Haifai akaacha kufanya matendo kwa ajili kuogopa asijionyeshe. Asiache matendo. Bali ajitahidi kufanya matendo mema na wakati huohuo apambane na nafsi yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21912/ما-حكم-ترك-العبادة-خوف-الرياء
  • Imechapishwa: 01/10/2022