Swali: Ni sahihi kwamba hakuna usengenyi kwa mtenda dhambi? Ni mtenda dhambi yupi ambaye inafaa kumsengenya ikiwa kitendo hicho ni halali?

Jibu: Hii sio Hadiyth. Makusudio ya wenye kusema hivo ni kwamba inafaa kubainisha zile kasoro zilizoko kwa mtenda dhambi kwa ajili ya kumrekebisha. Lengo sio kufurahikia. Mtu pia anaweza kufanya hivo kwa ajili ya kutahadharisha naye ikiwa anachelea watu wasije kudanganyika naye. Hii ndio maana ya msemo huu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (74) http://binothaimeen.net/content/1733
  • Imechapishwa: 29/08/2020