Usahihi wa ijumaa iliyotolewa Khutbah mojama

Swali: Wiki iliyopita mmoja katika maimamu alitoa Khutbah moja tu katika swalah ya ijumaa, kisha akaswali Rak´ah mbili na watu wakaondoka. Halafu wakatofautiana baada ya hapo kuhusu usahihi wa swalah hiyo. Je, inapaswa kurudiwa na kuswali tena pamoja na imamu huyu?

Jibu: Ndiyo, inapaswa airudie kama swalah ya Dhuhr. Miongoni mwa masharti ya swalah ya ijumaa ni Khutbah mbili, kama alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Isitohe amesema:

“Swalini kama mlivyoniona nikiswali.”

Allaah amsifu na amsalimishe!

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31567/هل-تصح-صلاة-الجمعة-بخطبة-واحدة
  • Imechapishwa: 06/11/2025